19 Machi 2011 - 20:30

Watu wasiopungua 12 wameuawa katika machafuko ya kidini yaliyowahusisha Waislamu na Wakristo katika eneo linalotenganisha kaskazini na kusini mwa Nigeria.

Msemaji wa jeshi la Nigeria Kapteni Chalres Ekeocha amesema machafuko hayo yalianzia katika eneo la Barkin Ladi kwenye jimbo la Plateau na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuchumwa nyumba za raia.Watu walioshuhudia pia wamesema shule za Kiislamu na makanisa mayeteketezwa kwa moto katika machafuko hayo. Jeshi la Nigeria limetangaza sheria ya kutotoka nje kwa muda wa masaa 24 katika eneo hilo ili kujaribu kudhibiti hali ya mambo.Mapigano ya jana yametokea baada ya siku tatu za machafuko yaliyosababisha vifo vya watu saba.Maelfu ya watu wameuawa katika machafuko ya kidini kwenye jimbo la Plaetau nchini Nigeria kwenye miaka ya hivi karibuni.